Template:Appeal/default/sw

From Donate
Jump to navigation Jump to search

Ombi kutoka kwa Jimmy Wales, mwanzilishaji wa wikipedia

Google ina mashine za seva milioni 1, Yahoo wana wafanyakazi 13,000. Sisi katika Wikipedia tuna seva 679 na wafanyakazi 95 pekee.

Wikipedia ni tovuti ya tano duniani kwa hesabu ya kutembelewa. Kila mwezi watu milioni 470 hutembelea tovuti yetu – wakiangalia mabilioni ya kurasa zetu.

Si vibaya kufanya biashara au kuonyesha matangazo ya kibiashara – lakini hapa Wikipedia hatutaki kufanya hivyo.

Wikipedia ni mahali pa pekee kwenye intaneti. Ni mahali kama maktaba au bustani yaani mahali ambako roho ya mtu inaweza kutafakari, kujifunza na tunapoweza kushirikiana na watu wengine ujuzi na maarifa.

Nilipoanzisha Wikipedia ingekuwa rahisi kuijenga kama biashara na tovuti inayozalisha pesa nyingi kwa njia ya kuonyesha matangazo ya kibiashara. Lakini sikutaka. Kwa hiyo tumejenga Wikipedia kwa pesa kidogo hasa kwa kujitolea na zawadi za wachangiaji. Usimamizi wa mitambo unaendeshwa na watu wachache sana. Ofisi ya Wikipedia haikuweza kunenepa – wanenepe wengine!

Kama kila msomaji angetoa dola tano kila mwaka kwa matumzi yake ya Wikipedia tusingehitaji kuomba kitu. Lakini si wote wanaoweza au wanaotaka kujitolea kwa njia hii. Hata hivyo tumepata wasaidizi wa kutosha hadi sasa.

Kwa sababu hii ninakuomba: usaidie na wewe mwaka huu. Ujitolee kwa dola $5, $10, $20 au jinsi unavyoweza. Tuendelee kujenga Wikipedia.

Ahsante sana

Jimmy Wales
Mwanzilishaji wa Wikipedia