Changia sasa
Maombi kutoka kwa Jimmy Wales, mwanzilishi wa Wikipedia.
Si vibaya kufanya biashara au kuonyesha matangazo ya kibiashara – lakini hapa si mahala pake. Siyo katika Wikipedia.
Wikipedia ni kitu maalumu. Ipo kama maktaba au mahali pa umma. Pako kama hekalu la maarifa. Ni mahali ambapo wote twaweza kwenda na kutafakari, kujifunza, na kuwagana maarifa yetu na wengine.
Nilipoanzisha Wikipedia ingekuwa rahisi kuijenga kama biashara na tovuti inayozalisha pesa nyingi kwa njia ya kuonyesha matangazo ya kibiashara. Lakini sikutaka. Kwa hiyo tumejenga Wikipedia kwa pesa kidogo hasa kwa kujitolea na zawadi za wachangiaji. Usimamizi wa mitambo unaendeshwa na watu wachache sana. Ofisi ya Wikipedia haikuweza kunenepa – wanenepe wengine!
Kama kila msomaji angetoa $5 kila mwaka kwa matumzi yake ya Wikipedia tusingehitaji kuomba kitu. Lakini si wote wanaoweza au wanaotaka kujitolea kwa njia hii. Hata hivyo tumepata wasaidizi wa kutosha hadi sasa.
Kwa sababu hii ninakuomba: usaidie na wewe mwaka huu. Ujitolee kwa dola 5, 10, 100 au jinsi unavyoweza. Tuendelee kujenga Wikipedia.
Ahsante sana,
Jimmy Wales
Mwanzilishi wa Wikipedia