Template:Appeal/default/sw

From Donate
Revision as of 01:26, 8 November 2011 by Jsoby (talk | contribs) (1 revision: importing old Jimmy translations for languages that don't have the new one translated)
Jump to navigation Jump to search

Mimi ninajitolea.

Silipwi hata senti kwa kazi yangu katika Wikipedia, na wala si hao wahariri na watunzi wengine wanaojitolea kufanya kazi katika Wikipedia. Nilipoanzisha Wikipedia, ningeweza kuifanya iwe kampuni ya kujipatia faida kwa kuweka mabango ya matangazo ya biashara, lakini niliamua kufanya kitu tofauti.

Biashara ni nzuri. Kutangaza si uovu. Lakini hapa si mahala pake. Sio katika Wikipedia.

Wikipedia ni kitu maalumu. Ni kama maktaba au hifadhi ya umma. Ni kama vile hekalu kwa ajili ya mawazo. Ni mahali ambapo wote tunaweza kwenda na kutafakari, kujifunza, kupeana maarifa yetu na wengine. Ni mradi wa kipekee wa kibinadamu, wa kwanza katika historia ya mwanadamu. Ni mradi wa kibinadamu unaoleta kamusi elezo huru kwa kila mtu katika dunia.

Kila mtu mmoja.

Iwapo kila mmoja anayesoma hii akangachangia $5, tungeweza kumaliza uchangishaji leo hii. Lakini si kila mtu anaweza au atachangia. Na kwa hilo ni sawa tu. Kila mwaka watu wanaoamua kutoa wanatosha. Tukifikia lengo, tunasimamisha kampeni hizi. Sisi ni shirika dogo, na nimefanya kazi kwa juhudi kwa zaidi ya miaka kadhaa ili kutuweka katika hali inayofaa. Tunatimiza mpango wetu, na kuacha yasiyofaa kwa wengine.

Kutimiza mipango yetu bila kuweka matangazo, tunakuhitaji wewe. Ni wewe unayeweka ndoto hii hai. Ni wewe uliyeanzisha Wikipedia. Ni wewe unayeamini ya kwamba kuna haja ya kuwa na sehemu ya kutafakari na kujifunza kwa utulivu.

Mwaka huu, tafakari kufanya mchango wa $5, $20, $50 au kiasi chochote unachoweza kuilinda na kuiendeleza Wikipedia.

Ahsante,

Jimmy Wales

Mwanzilishi wa Wikipedia