Template:Appeal/Isaac/sw

From Donate
Jump to navigation Jump to search

Kutoka kwa mhariri wa Wikipedia Isaac Kosgei

Maarifa ni ya kila mtu, hata wale bila mtandao wa intaneti. Siku hizi, mashule mengi Kenya yana tarakilishi. Lakini mengi bado hayana intaneti, sana sana mle vijijini katika nchi langu.

Kama mhanag wa Wikipedia, mchango wangu kuu ni usamabzaji wa toleo ya Wikipedia isiyohitaji intaneti. Toleo hili ni la maandishi pekee.

Kusafiri kwa basi na teksi, huku tukiwa tumejiami kwa diski-ROM, diski-USB, kompyuta ya mkononi na projector, mie na rafiki zangu hutembele mashule Kenya kote.

Sisi husakinisha Wikipedia katika makompyuta ya shule na kuwaelimishawalimu ambavyo mradi unavyoendeshwa. Kisha tunaipa shule mzima mifano tukitumia projector na kupeana hotuba wa umuhimu wa wikipedia

Walimu wanasema ya kwamab mradi huu umebadili maisha ya maelfu ya wanafunzi na unaleta mapinduzi katika elimu nchini kenya. Wanafunzi huwa wenye furaha na hutushukuru kwa vitendo hivi.

Kutokana na wikipedia - na safari kadha refu katika mabasi yaliyojawa na vumbi - kizazi kizima cha wanafunzi sasa kina kamusi elezo kubwa zaidi duniani. Ninavyoona, hichi ndicho jambo bora zaidi kutendeka.

Unapochangia kwa Wikipedia, wabadilisha dunia. Kutoka kwa mvunguni mwa moyo wangu, asante.

Isaac Kosgei
Mwanafunzi wa Biashara na muhanga wa Wikipedia